Business

header ads

MACHALI AHAMIA CCM KUUNGA MKONO JUHUDI ZA DKT. MAGUFULIAliyekuwa Mbunge wa Kasulu kupitia NCCR-Mageuzi, Moses Machali amehamia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha ACT-Wazalendo ili aunge mkono jitihada za utendaji kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

Katika taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana, ambayo mwanasiasa huyo amelithibitisha kuwa ni yake, alisema ni aibu kwa mtu yeyote makini na anayehitaji mabadiliko kushindwa kuunga mkono jitihada za Dk Magufuli.

Alisema kuwa yeye ameamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi ,

Mimi niliyefanya sana siasa za upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ” alisema Machali.

Alisema watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga Tanzania kwa maendeleo endelevu ni jamii ya viongozi kama Dk Magufuli, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, mawaziri na viongozi wengine walioko chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Machali aliyeanza safari yake ya siasa tangu mwaka 2007 hadi 2010 akiwa Chadema, 2010 hadi 2015 akiwa NCCRMageuzi na 2015 hadi 2016 alipojiunga na ACT na sasa CCM, alisema mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake unatosha kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono.

Mimi nimechagua kumuunga mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma rekodi yangu ya enzi nikiwa mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge nilipinga mno wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa,” alisisitiza.

Alisema kutokana na jitihada zake kwa kushirikiana na wabunge wengine wa upinzani katika kupinga ufisadi, leo Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha kasi nzuri katika kuwachukulia hatua watu hao. “Hata hivyo, leo hii upinzani umepoteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ilichokihubiri nchini.
SOURCE: HABARI LEO

Post a Comment

0 Comments