Business

header ads

Kaya 42,000 zaondolewa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini

Zaidi ya KAYA 42,000 zimeondolewa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania zikiwemo kaya hewa 11,212 kutokana na uhakiki uliofanyika kuanzia Februari hadi Oktoba mwaka huu ili kuziondoa kaya ambazo hazina sifa.

Takwimu hizo zilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki wakati akifungua kikao cha kazi kilichohudhuriwa na wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka mikoa wa Rukwa na Katavi kilichofanyika jana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Waziri Kairuki alisema , kati ya hao, waliokufa ni kaya 10,424, viongozi 3,745 waliohama sehemu ambapo mpango huo haujaanza 5,267 na wasiokuwa na sifa 11,387.
Alisema katika uhakiki huo kaya 866 zikiwemo kaya hewa 195 zimeondolewa katika mpango huo katika mikoa ya Rukwa na Katavi. Kwa wastani kaya moja hulipwa kati ya Sh 20,000 hadi 60,000 kwa kutegemea idadi ya watu katika kaya.

Aidha, Kairuki ameagiza watumishi wote waliosababisha matumizi mabaya ya fedha kwa kuwaingiza walengwa wasiostahiki katika mpango huo unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) Awamu ya Tatu wachukuliwe hatua za kinidhamu na kijinai kwa lengo la kukomesha tabia hizo.

Post a Comment

0 Comments