Business

header ads

DONALD TRUMP AWA RAIS WA 45 WA MAREKANI

Donald Trump amemshinda Mgombea wa Democratic Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali na kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Katika uchaguzi huo Bw Trump ametajwa kushinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi wake. Majimbo hayo ni pamoja na Ohio, Florida, na North Carolina, huku  Bi Clinton akishinda katika jimbo la  Virginia.
Chama cha Republican pia kimehifadhi wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.
Baada ya matokeo hayo Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.
Donald Trump anakuwa rais wa 45 wa Marekani akipokea kutoka kwa rais Baraka Obama. Anatarajiwa kuapishwa ifikapo January 20, 2017.
HISTORIA YA DONALD TRUMP
DONALD TRUMP JOHN alizaliwa 14 Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.
Upande wa baba yake (Fred Trump aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake (Mary) ni mzaliwa wa Scottish.
Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambako alihitimu shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.
Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ambayo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu.
Trump ambaye ni baba wa watoto watano, ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.
Baadhi ya mali anazomiliki
Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama, Trump Tower lililopo Manhattan, Wollman Rink lililoko Central Park,Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey,Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland
Trump Hotel Las Vegas, Trump International Hotel & Tower ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Chicago, Trump International Hotel ya Las Vegas, Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk
Trump SoHo ya New York, Trump International Hotel & Tower ya Toronto, Taasisi ya Donald J. Trump Branding na licensing, Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.
Utajiri
Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni 3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi kwenye historia ya nchi hiyo.
Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake (brand), Trump anakadiliwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 .

Post a Comment

0 Comments