Business

header ads

 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 2016

  Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 2016.PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli ambaye pia niAmiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama leo amewatunukia kamisheni maafisa wanafunzi wa kijeshi 194 katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam..

Katika sherehe hizo rais alikagua Grwaride kabla ya kuwatunukia kamisheni maafisa hao na baadae kushuhudia gwaride la kimywa kimywa lililoonyeshwa na askari kutoka kambi ya Abdalah Twalipo ya jijini Dar es salaam na kisha bendi ya jeshi hilo kupita mbele ya amiri jeshi mkuu ikiwa ni sehemu ya Burudani ya sherehe hizo.

Kamisheni hiyo ni ya 59 ya maafisa wanafunzi wa jeshi kutunikiwa baada ya mafunzo ya mwaka mmoja katika chuo kikuu cha maafisa wa kijeshi Monduli Mkoani Arusha na ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na maafisa waandamizi wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania

Post a Comment

0 Comments