Business

header ads

ABIRIA WATAKIWA KUTOA TAARIFA KUHUSU MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA

 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewaasa abiria kutoa taarifa pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao katika vyombo vya usafiri.
Masauni ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani cha ubungo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.

Masauni amesema dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani na kuwa abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.

Post a Comment

0 Comments