Business

header ads

WAZIRI NAPE AWASILISHA SHERIA YA HUDUMA ZA HABATI KWA KAMATI YA BUNGEWaziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Nnape Nnauye amewasilisha mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii,muswada wa sheria huduma za habari wa mwaka 2016 huku wanataaluma ya habari wakitakiwa kufuata weledi na maadali ya fani hiyo kwa kuepuka uchochezi unaoweza kuligharimu taifa

Muswada wa sheria za huduma za habari umeandaliwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika tasnia ya habari nchini,ambapo miongoni mwa changamoto ni pamoja na upungufu wa sheria zinazosimamia tasnia ya habari na mabadiliko ya teknolojia ya habari,uchumi,siasa na jamii

Akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya huduma na maendeleo ya jamii waziri nape nnauye amesema kupitia muswada huo utasaidia kuifanya sekta ya habari kuwa taaluma kamili na itawezesha kwa mfumo mzuri wa usimamizi wa tasnia hiyo

Aidha nape akawataka wanahabari na wadau wa tasnia ya habari kuendelea kutoa maoni kabla muswada huo haujafikishwa bungeni kwa lengo la kuuboresha.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii wamedai muswada huo utawezesha kuilinda tasnia ya habari kwa maslahi mapana.

Post a Comment

0 Comments