Business

header ads

WAZIRI MKUU ATAKA MJI WA DODOMA KUWA TOFAUTI NA MIJI MINGINEWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mji wa Dodoma ni lazima upangwe ili uwe tofauti na miji mingine hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini jijini Dar es Salaam na kuelezea nia yake ya kutaka kuwekeza mjini Dodoma ambapo amesema Serikali haitaki kurudia makosa yaliyofanyika kwenye miji mingine.


Amesema ni lazima mji upangwe kama ambavyo miji mingine mikuu inapangwa. Na kuwa serikali haiwezi kuachia watu wajenge popote na wanavyotaka, ambapo matokeo yake miji mingi inakuwa katika mipangilio mibaya na kuwa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya kuhamia Dodoma imepewa jukumu la kupitia upya Master Plan ya mji wa Dodoma na kuainisha maeneo ambako nyumba za aina mbalimbali zitajengwa.


Akizungumzia kuhusu ujenzi kwenye maeneo ambayo tayari wananchi wanaishi, Waziri Mkuu amesema Serikali itaweka utaratibu ili kuwe na mikataba baina ya mwekezaji na mwananchi anayemiliki eneo husika ili asinyimwe haki ya kumiliki eneo lake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali katika zoezi la Serikali kuhamia Dodoma kwa lengo wa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata makazi bora na ya kudumu.

Post a Comment

0 Comments