Business

header ads

WATENDAJI WANAORUDISHA NYUMA JITIHADA ZA UANZISHAJI VIWANDA KUKIONA


Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema kwamba serikali itawachukulia hatua kali watendaji wabadhilifu na watakaobainika kuhujumu juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuanzisha na kufufua viwanda vipya zinazoongozwa na Rais Dakta John Pombe Magufuli  katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo katika mkutano Mkuu wa sita wa wadau wa Mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF unaofanyika jijini Arusha na kuainisha kuwa viwanda vingi vimekufa kutokana na uwajibikaji mbovu wa watendaji wa Serikali ambao hawatavumiliwa katika awamu hii.

Katika ufunguzi wa mkutano huo Waziri Mkuu amesema Serikali tayari imeshalipa zaidi ya shilingi bilioni 700 kati ya shilingi billioni 964.2 za madeni ya michango ya jumla ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Post a Comment

0 Comments