Business

header ads

WATAHINIWA 238 WAMEFUTIWA MATOKEO YAO YA DARASA LA SABASerikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema ya mkoani Shinyanga.
Akitangaza matokeo hayo leo , Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani, NECTA, Dk Charles Msonde amesema jumla wa watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu.
Amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 70.3 ya ufaulu tofauti na ufaulu wa mwaka jana ambao ulikuwa ni asilimia 67.8
Aidha, Dk. Msonde amesema jumla ya watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu, huku shule 6 waalimu, wamiliki wa shule na wasimamizi wa mitihani wakibainika kufanya udanganyifu na kuwafanyia mtihani wanafunzi.
Amesema katika mtihani huo mwaka huu jumla ya watahiniwa 795,739 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wasichana 422,864. sawa na asilimia 53.14 na wavulana 372,875 sawa na asilimia 46.86. Watahiniwa 789.479 sawa na asilimia 99.21 ya waliosajiliwa walifanya mtihani. wasichana wakiwa 419.932 sawa na asilimia 99.31.wavulana walikuwa 369.547 sawa nasilimia 99.11

Post a Comment

0 Comments