Business

header ads

WANAWAKE WANAFANYA KAZI DK 50 ZAIDI YA WANAUMERipoti iliyotolewa na Jukwaa la Uchumi Duniani, WEF, imesema wanawake wanafanyakazi wastani wa siku 39 zaidi kwa mwaka kuliko wanaume.

Ripoti hiyo inayojulikana kama Global Gender Report, imesema pia wanawake wanafanyakazi wastani wa dakika 50 zaidi kwa siku kuliko wanaume.

Imesema wanawake wanabeba mzigo wa kufanya kazi bila malipo na inakadiria kwamba, itachukua miaka 170 kuziba pengo la tofauti za kiuchumi kati ya jinsia hizo mbili ambapo pengo hilo ni kubwa sasa kuliko wakati wowote tangu mwaka 2008.

Vesselina Ratcheva, mchambuzi wa takwimu wa Jukwaa la Uchumi, amesema, likizo za pamoja za uzazi zinaweza kuwa nzuri kwa sababu zinawezesha familia kupanga maisha yao, idadi ya watoto pamoja na kugawana majukumu.

Bi Ratcheva amesema likizo za aina hiyo zinaweza kutoa fursa pana zaidi kwa akina mama kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi na kujiingizia mapato ya ziada.

Post a Comment

0 Comments