Business

header ads

WAMAREKANI KUPIGA KURA MAPEMA KABLA YA UCHAGUZI

Maelfu ya Wamarekani tayari wamewapigia kura Hillary Clinton, Donald Trump au wagombea wengine wa Urais kabla ya siku ya uchaguzi mkuu Novemba nane , ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa kura za mapema ambao sasa umejipatia umaarufu.
Zikiwa zimesalia siku 35 kabla ya uchaguzi huo, Profesa Michael McDonald wa Chuo Kikuu cha Florida anasema takriban watu 130,000 tayari wamepiga kura kati ya wapiga kura milioni 130 wanaotarajiwa.
Kura hizo zitahesabiwa rasmi siku ya uchaguzi Jumanne Novemba 8, ambapo mfumo wa upigaji kura nchini Marekani umeunganishwa huku majimbo 50 yakiandaa utaratibu wa upigaji kura na kila jimbo huhesabu kura peke yake.

Kura za mapema hupigwa kwa njia mbili kwa barua pepe na kwa mtu mwenyewe kwenda katika kituo cha kupigia kura.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Sensa ya Marekani upigaji huo wa kura unazidi kupanuka ambapo mwaka 1996 10.5% ya kura zilizpigwa mapema na mwaka 2012 idadi hiyo iliongezrka na kufikia theluthi.

Post a Comment

0 Comments