Business

header ads

WALIOHUSIKA NA TUKIO LA KUMPIGA KIKATILI MWANAFUNZI KUFUKUZWA CHUO
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewafukuza chuo walimu wanafunzi WATATU kwa tuhuma za kumpiga mwanafunzi Sebastian Singuli.

Profesa Ndalichako amesema kwa mujibu taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanywa na wanafunzi hao ni kosa la jinai na hawawezi kuendelea na taaluma ya ualimu kwa sababu wamekosa sifa ya kuwa walimu.

Aidha ameelezea kusikitishwa kwake pamoja kuchukizwa na kitendo hicho ambacho amesema si cha kawaida na hakiwezi kufumbiwa macho.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makalla, amesema tukio hilo lilitokea Septemba 28, baada ya mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu kugoma kufanya adhabu ya kupiga magoti na push up aliyopewa na Mwalimu Frank Musigwa.
Baada ya kusambaa kwa video hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba, ameviagiza vyombo vya dola kufuatilia tukio hilo ambapo Mkuu wa shule hiyo na baadhi ya waalimu wamechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.

Post a Comment

0 Comments