Business

header ads

WADAU WA HABARI WAPEWA SIKU SABA KUWASILISHA MAONI YA MUSWAADA WA YA HABARI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imetoa siku saba zaidi kwa wadau mbalimbali wa Habari ili kusoma  Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuwasilisha maoni yao kwa kamati hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Peter Serukamba alipokuwa akitoa marejesho kwa Waandishi wa Habari  ambapo amesema licha  ya kupewa zaidi ya mwezi mmoja tangu Bunge lilipoweka hadharani muswaada huo lakini wadau hao wameshindwa kuwasilisha maoni yao kwa kamati kwa madai ya kutousoma na hivyo kulazimika kupewa siku saba zaidi.

“Niwapa wadau wiki moja wawe wameleta maoni yao kwa maandishi yaani mpaka Jumatano ya wiki ijayo wawe wameyawasilisha kwa Kamati kwa kuwa leo tumewaita wakasema hawakupata muda wa kusoma,” alisisitiza Mhe. Serukamba.

Mhe. Serukamba ameongeza kuwa mchakato wa kuunda sheria unashirikisha wadau husika kwa kuleta maoni yao juu ya Mswada husika na maoni yao yanasaidia katika kutengeneza sheria iliyo nzuri kwa ajili ya Tasnia ya Habari na maendeleo yake kwa ujumla.

Ameeleza kusikitishwa na wadau hao kushindwa kusoma muswada huo au kuonekana wana ajenda yao na kusisitiza kuwa anaamini kwa muda ambao Kamati imetoa kwa wadau kuwasilisha maoni yao kwa kamati watakuwa wamewasilisha maoni kwa wakati ila kamati iyapitie kabla ya kupelekwa kwa Spika wa Bunge na kuanza kujadiliwa Bungeni.

Miongoni mwa wadau waliofika lakini wakashindwa kuwasilisha maoni ni Jukwaa la Wahariri, Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MoAT), Chama cha Wanasheria Nchini na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini.

Post a Comment

0 Comments