Business

header ads

TFDA YAKAMATA DAWA BANDIA AINA TANOMamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewataka watoa huduma za afya na wafanyabiashara za dawa kote nchini  kurudisha dawa za malaria  pamoja dawa za viuavijasumu (Antibiotic) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17 ambazo zimebainika kuwa ni bandia kutokana zoezi ukaguzi lililofanywa na mamlaka hiyo.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Silo ametaja baadhi ya  dawa hizo kuwa  ni vidonge vya aina ya Eloquine,quinine Sulphate 300mg ambazo hutibu malaria ,  Erythromicin, Doxycyline 100mg na Siproflaxine  pamoja na ambazo hutumika kama viuajisumu zilizokamatwa katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Mara, Geita na Shinyanga.Amesema Uchunguzi wa awali umeonesha kwamba dawa hizi bandia zinatengenezwa hapa nchini katika makazi ya watu na maeneo mengine ya kificho ambapo dawa zilizoisha muda wa matumizi huongezwa muda kwa kuondoa lebo za zamani na kubandika mpya.

Bw. Sillo ametaja maeneo yaliyohusika na ukaguzi huo ni pamoja na famasi, maghala ya dawa, zahanati, maduka ya dawa za mifugo pamoja na maduka ya dawa muhimu ambapo jumla ya maeneo 207 katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Mara, Simiyu, Geita na Shinyanga yalikaguliwa kwa idadi kama ifuatavyo; Mbeya (70), Songwe (34), Mara (25), Simiyu (34), Geita (33) na  Shinyanga (11).

Post a Comment

0 Comments