Business

header ads

SERIKALI YAWAFUTIA HATI ZA UMILIKI WA ARDHI WALIOKIUKA MASHARTISerikali ya Tanzania kupitia wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi imefuta umiliki wa kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye kilichopo Tegeta kutokana na kushindwa kuendeleza kwa muda na baadae kuvamiwa na wananchi.Pia Serikali imefuta hati tano za umiliki wa ardhi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na raia wa Uingereza aliyetajwa kwa jina la Hamant Patel mkazi wa Mwanza baada ya kugundulika kughushi cheti cha kuzaliwa na kujitambulisha kama raia wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema hati hizo zilizofutwa zilitolewa kwa udanganyifu kwa mmiliki huyo katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu.

Aidha waziri Lukuvi ameongeza kuwa watu wenye uraia wa nje ni watanzania hawana uwezo kupata ardhi nchini na wanachotakiwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) ndio wanaweza kutoa ardhi.Kwa upande mwingine serikali imetoa miezi mitatu kwa watu wanaomiliki viwanja kwa ofa ya jiji ili kuweza kupata hati baada ya kubainika kuwepo kwa matapeli wa kugushi nyaraka za serikali kwa viwanja hivyo.

Waziri Lukuvi amesema serikali haitaangalia mtu mtu usoni kwa watu kumiliki ardhi bila kuendeleza kwa muda mrefu huku kukiwa na viwanja vingine kukosa mapato yake.

Post a Comment

0 Comments