Business

header ads

SERIKALI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHA WADOGO TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inayafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara juu ya kuwepo kwa mlolongo mkubwa wa kodi hivyo amewataka kuwa watulivu wakati huu serikali ikishughulikia malalamiko hayo.

Makamu wa Rais amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizindua Jumuiya ya wanawake wajasiriamali na biashara Kariakoo JUWABIKA uzinduzi ulioenda sambamba na kuzindulikuwa kwa katiba watakayotumia wafabiashara hao.

Amesema kuwa majukwaa hayo yatazinduliwa nchi nzima ili kuweza kuanisha vipaumbele, huhudi,mafanikio na changamoto za kumuendeleza na kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Ameongeza kuwa serikali inatambua ugumu uliopo kwa wafanyabiashara wadogo kupata mikopo ya kujiendeleza kutoka katika mabenki na taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo riba kubwa na masharti magumu na kuwa imeandaa mpango wa kurasimisha na kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanya biashara na kupata mikopo yenye masharti nafuu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya wanawake na maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete amewataka wanawake hao kujiamini kwa kile wanachokifanya katika kukuza na kujiendeleza kiuchumi badala ya kujiona kama hawawezi

Post a Comment

0 Comments