Business

header ads

PICHA ZA TUKIO LA DHIFA YA TAIFA KWA RAIS KABILA IKULU

  Rais Joseph Kabila akimwamkia Mama Sitti Mwinyi, Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi,  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake

 Rais Dkt Magufuli akiwa meza kuu na mgeni wake Rais Joseph kabila na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wafanyabishara maarufu nchini Saidi Salim Bakhressa (kushoto) na Mohamed Dewji
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisimua wasikilizaji wa hotuba yake
  Mwanamuziki Christian Bella akitumbuiza kwenye dhifa hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila wakiongea na mawaziri wao wa nchi za nje  Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma mbele ya Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwa heshima yake. 
PICHA NA IKULU

Post a Comment

0 Comments