Business

header ads

MIKATABA 21 YASAINIWA KUWASILI KWA MFALME WA MOROCCO TANZANIA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakipita katika gadi ya mapokezi iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakilakiwa na wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ujio wa Mfalme wa Morocco nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kibiashara na uwekezaji kwa Tanzania na Morocco ambapo Tanzania imesaini mikataba21 ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco Mohammed VI ambapo amesema Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji pamoja na kuainisha mambo mbalimbali katika mazungumzo yao ikiwemo uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini, uwekezaji utakaosaidia kukuza pato la taifa.

Akitaja baadhi ya makubaliano ni pamoja mfalme Mohamed VI kuihakikishia nchi kuwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Rabat Morocco hadi Dar es salaam Tanzania, kutolewa nafasi kwa Askari wa Tanzania takribani 150 watakaokwenda kujifunza masuala ya ulinzi na usalama nchini Morocco.

Akiyataja mengine ni pamoja na Mfalme wa Morocco kukubali kujenga Msikiti mkubwa na uwanja wa mpira DodomaPost a Comment

0 Comments