Business

header ads

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU ATAKA KAMPENI YA UPANDAJI MITI IFANYIKE NCHI NZIMA


Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kampeni ya upandaji miti ilioanza leo kwa mkoa wa Dar es salaam haina budi kufanyika nchi nzima ili kuhakikisha nchi inakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo kkatika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

Amesema ni matumaini yake kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.


Kwa upande wao waziri wa mazingira na muungano Mh. Januari Makamba pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wamesema wananchi hawana budi kuitunza miti hiyo waliyoipanda ili isiharibike.

Uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam,ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi.Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments