Business

header ads

MAKAMU WA RAIS ALAANI MAUAJI YA WATAFITI DODOMAMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelalani vikali mauaji ya watafiti wawili wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na dereva mmoja waliokuwa kazi katika kijiji cha Mvumi Makulu wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kongamano ya 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambapo amesema kuwa tukio hilo ni baya na amewahakikishia watafiti wanaoshiriki kongamano hilo kuwa serikali itachukua hatua stahiki kwa watu  waliofanya kitendo hicho cha kinyama ili kukomesha tabia hiyo.

Haiwezekani hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria alisisitiza Makamu wa Rais”


Akizungumzia masuala ya utafiti, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo serikali itaendelea kutoa mchango wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa.

Makamu wa Rais pia amewahimiza wafadhili waendelee kusaidia watafiti hasa wanaofanya tafiti za afya nchini kwa sababu tafiti hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema kuwa watafiti wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti zao nchini hivyo jitihada hizo ni muhimu zikaimarishwa ipasavyo.


Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments