Business

header ads

MAKAMPUNI 82 YAKIUKA MKTABA WA UENDESHAJI NA NJONANJE SAMWELI
Uchambuzi uliofanywa na ofisi ya Msajili wa Hazina nchini imebaini uwepo wa takribani makampuni 82 ambayo yamekiuka mikataba ya uendeshaji wa makampuni ya umma waliyouziwa kwa njia ya uwekezaji na kwamba makampuni hayo yamekabidhiwa serikali kwa ajili ya maamuzi ya mwisho ikiwa ni pamoja na kutafutiwa wawekezaji wapya.

Msajili wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amesema hayo leo katika mahojiano na EATV na kufafanua kuwa idadi hiyo ni sehemu tu ya makampuni yote ambayo wamiliki wake walitakiwa kupeleka taarifa ya hali halisi ya uendelezaji wa miradi hiyo baada ya kubinafsishwa, taarifa iliyokuwa na lengo la kubaini iwapo uendelezaji unaofanywa kwenye mashirika hayo ya umma inalinufaisha taifa.

Bw. Mafuru ameyataja baadhi ya mashirika na makampuni ambayo baraza la mawaziri litapitia taarifa zake na kutolea maamuzi kuwa ni pamoja na kiwanda cha nguo cha Urafiki, shamba la chai la Mponde lililopo Lushoto mkoani Tanga pamoja na kiwanda cha matairi cha General Tyre.

Post a Comment

0 Comments