Business

header ads

ITALIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA


Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni ameahidi nchi yake kuendelea kudumisha na kukuza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi yake na Tanzania katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Balozi Roberto Mengoni ametoa kauli hiyo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini na kusema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya nchi hizo.

Post a Comment

0 Comments