Business

header ads

IDADI YA WATOTO WA MTAANI YAONGEZEKA MKOANI MWANZAImeelezwa kuwa idadi ya watoto wa kike wanaohusishwa kwenye shughuli za kingono Mkoani Mwanza wenye umri kati ya miaka 11 hadi 14 imeongezeka huku watoto 1,940 wanaishi mitaani na kufanya kazi katika jiji hilo.

Takwimu hizo zimetolewa na mashirika yanayo jishugulisha na watoto wa mitaani ya Railway Children Africa pamoja na JUCONI baada ya kufanya utafiti kwa miezi 12 jijini humo na kubaini kuwa asilimia 100 ya watoto wote wa mitaani wanaambiwa maneno yasiyo faa huku asilimia 97 kati yao wa kike na wakiume wakiwa wamedhalilishwa kijinsia na kubakwa

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Railway Children Africa, Bw. Pete Kent, amesema, kuna uwezekano mkubwa watoto wa mitaani kutonufaika na Malengo Endelevu ya Maendeleo, SDG kutokana na kutengwa na jamii hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuvunja mzunguko wa ukatili dhidi yao.

Post a Comment

0 Comments