Business

header ads

ELIMU YA TEKINOLOJIA KUWASAIDIA WACHIMBAJI MADINI

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito kwa wachimba wadogo wadogo wa madini kuongezea juhudi katika uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu ya uchimbaji sahihi wa madini na kutumia teknolojia nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao.

Profesa Ntalikwa ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo  ambapo amewasihi kupata elimu na teknolojia sahihi ili waweze kujiongezea kipato katika uchimbaji huu.

Aidha Katibu Mkuu uyo aliwataka wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala la mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.

Pia amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa wachimbaji hawa wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu ya ruzuku ikiwa na lengo ya kuwasaidia kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kwa sasa wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji mbalimbali na wanayafanyia kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.

Post a Comment

0 Comments