Business

header ads

AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA KWA ASILIMIA 10


Takwimu za mkakati wa kupunguza ajali kwa asilimia 10 kwa kipindi cha miezi sita zinaonyesha kuwa kwa miezi miwili kabla ya kuanza kwa mkakati huo kulitokea ajali 577 na miezi miwili baada ya kuanza kwa mkakati huo zilitokea ajali 471.

Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama barabarani Mhandisi Hamad Masauni wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa barabara la taifa la usalama barabarani Tanzania bara wa kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 10 kwa kipindi cha miezi 6 iliyojiwekea.

Kulingana na takwimu hizo zinaonyesha kuwepo kwa upungufu wa ajali 106 ambazo ni sawa na asilimia 18, aidha katika kipindi hicho cha miezi miwili kabla ya mkakati kulitokea vifo 467 na baada ya mkakati kulitokea vifo 91 ambavyo ni sawa na asilimia 19.

Mhandisi Masauni amesema pia kwa kipindi hicho , miezi miwili kabla ya mkakati kulitokea majeruhi 810 na baada ya mkakati kulitokea majerughi 49, takwimu hizo zinaonyesha kuwepo kwa upungufu wa majeruhi 314 ambao ni sawa na asilimia.

Post a Comment

0 Comments