Business

header ads

WENYE VYETI FEKI WATAKIWA KUJISALIMISHA

Baraza la Mitihani nchini  limesisitiza  kwa watumishi wa umma na wasiokuwa wa umma wanaotumia vyeti vya kughushi au vya watu wengine kujisalimisha kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde, amesema, katika zoezi linaloendelea nchi nzima wamekamata watu wengi ambao ni watumishi wa umma wakiwa wameajiriwa hali ya kuwa wanatumia vyeti ambavyo si halali ama vya mtu mwingine.

Dk. Msonde ametumia fursa hiyo kuwataka watu wengine ambao wanajua wanafanya hivyo kujisalimisha wenyewe kujitoa wenyewe katika ajira badala ya kusubiri kuumbiliwa na serikali ambapo amesisitiza  wanafanya utaratibu wa kufuatilia suala hilo katika taasisi nyingine ambazo si za umma wala za kiserikali.

Post a Comment

0 Comments