Business

header ads

WAZIRI MAJALIWA AWASILI RASMI DODOMAWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amehamia rasmi mkoani Dodoma Ijumaa Septemba 2016.
Majaliwa ametua katika uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10.07 jioni akiwa ameongozana na mkewe na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Walemavu, Jenester Mhagama.

Baada ya kuwasili alikwenda moja kwa moja kwenye makazi yake mpya yalioko Mlimwa ambako alipokewa na wazee wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wa dini.

Katika Barabara inayoelekea kwenye makazi yake, wakazi wa Dodoma wamesimama kandokando wakimshangilia wakimpungia majani ya miti kama ishara ya amani huku katika lango la kuingilia nyumbani kwake, kukiwa kumejaa Bajaji na pikipiki.


Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments