Business

header ads

WATU 7 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 120 KUJERULIWA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji.
Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.
Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde.
Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la ardhiPICHA ZOTE NA BLOG YA HABARI360
 TAARIFA KAMILI Watu saba wamefariki Dunia katika Tetemeko la ardhi lilitokea leo Mkoani Kagera na kusababisha majeruhi zaidi ya 120 baada ya nyumba kadhaa kubomoka na kusababisha taharuki kubwa katika eneo hilo la kanda ya Ziwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu amesema kuwa maeneo yaliyoathirika ni katika wilaya zote za mkoa huo ikiwemo wilaya ya Bukoba, Karagwe,Kyerwa na nyinginezo.

 Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza kwa njia ya simu wamesema kuwa nyumba nyingi zimeharibiwa, huku mkuu wa mkoa akieleza kuwa wanakusanya taarifa za majeruhi na walifariki ili kutoa idadi kamili.

Post a Comment

0 Comments