Business

header ads

WATOTO ZAIDI YA 15,000 HUZALIWA NA TATIZO LA MOYO
Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto toka taasisi ya Jakata Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Godwin Godfrey, amesema takwimu zinaonesha kwamba,  watoto wengi hufariki kabla ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo bila kugundulika na kupatiwa matibabu ya haraka.

Dk .Godfrey  amesema hayo leo wakati akiongea na East Africa radio, ambapo amesema kwa mwaka jana pekee kuna watoto zaidi ya elfu 15 walizaliwa na tatizo la moyo lakini waliojitokeza kupatiwa matibabu hawafiki hata watoto mia mbili.

Dkt. Godfrey, amesema kuwa hali hiyo inatokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha hali ambayo inawafanya wazazi kuwapeleka watoto hao tayari ugonjwa ukiwa umeshawashambulia kwa kiasi kikubwa.

Post a Comment

0 Comments