Business

header ads

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA UTAMADUNI WA KUJITOLEA
Rais mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania Alhajj Ally Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuendeleza utamaduni wa kusaidiana katika majanga mbali mbali yanayotokea kwa kuwa hakuna binadamu au serikali yenye uwezo wa kufanya kila jambo bila ya kushirikiana na wananchi wake.

Rais huyo mstaafu wa awamu ya pili ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati wa matembezi ya hisani yaliyokuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambapo katika matembezi hayo zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu zilipatikana.

Alisema mshikamano baina ya watanzania wenyewe utasaidia kuleta faraja kwa wananchi wa Bukoba kutokana na sasa wengi wao kuishi katika hali ya kukosa matumaini

”Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema hakuna nchi yoyote duniani ambalo linafahamu siku ambayo tetemeko la ardhi linatokea na kupanga bajeti yake.

Tetemeko hilo lililotokea September 10 mwaka huu limesababisha  vifo 17, kuanguka kwa nyumba 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 pamoja na mali ya Taasisi za umma.

Post a Comment

0 Comments