Business

header ads

WAFUASI WA HILARY CLINTON WAMLAANI TRUMP

Wafuasi wa Bi Hillary Clinton, wamelaani vikali matamshi  ya kejeli aliyotoa Donald Trump, dhidi ya Bi Hillary Clinton.

Mgombea urais kupitia chama cha Republican,Donald Trump  amesema walinzi wa Bi Clinton wapokonywe silaha walizo nazo  kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na wafuasi wa Bi. Clinton.

Bwana Trump alikuwa akizungumza na wafuasi wake katika mkutano wa kampeni huko Miami ,akitetea hoja yake kwamba raia wa Marekani wana haki ya kumiliki bunduki.

Bw. Trump amedai  Bi Hillary Clinton anataka kuwaondolea sheria inayowapa haki hiyo Wafuasi wa Bi Clinton wanasema kauli hizo za Trump hazikubaliki kwani ni za kuchochea ghaisia.

Post a Comment

0 Comments