Business

header ads

VIJANA MILIONI MOJA KUINGIA KATIKA SOKO LA AJIRA SA

Serikali na sekta ya biashara nchini Afrika Kusini zimeridhia utekelezaji wa uanzishaji programu ya ajira kwa vijana wenye lengo la kuwachukua vijana milioni moja kwa mafunzo kazini kwa malipo katika sekta binafsi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Gharama za programu hiyo zitabebwa na sekta binafsi na itaungwa mkono na serikali kwa mazungumzo maalum ya utoaji wa bahashishi.

Taarifa za programu hiyo ya ajira kwa vijana imebainika baada ya kufanyika mkutano baina ya rais Jacob Zuma, Naibu wake Cyril Ramaphosa na Watendaji Wakuu wa Sekta Binafsi katika jengo la Umoja Jijini Pretoria.

Katika kufanikisha programu hiyo sekya binafsi pia imekusanya kiasi cha randi bilioni 1.5 za Afrika Kusini katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuimarisha biashara ndogo na za kati.

Post a Comment

0 Comments