Business

header ads

USHIRIKIANO TANZANIA, MSUMBIJI KUBORESHA MAENDELEO


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bibi, Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge Augusto Menezes.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio  mara  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
[Picha na Ikulu.]

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Msumbiji na Tanzania ni nchi zenye historia katika uhusiano na ushirikiano wao hivyo kuna haja ya kuendelezwa na kuimarishwa zaidi kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi mpya  wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniam Monica Patricio Clemente Mussa  aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbuji ni wa kihistoria ambao umeasisiwa na viongozi wa wa Mataifa hayo akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Samora Machel.

Akisisitiza juu ya uhusiano na ushirikiano wa kidugu kati ya Zanzibar na Masumbiji, Dk. Shein alisema kuwa katika kuliimarisha hilo Zanzibar hivi sasa kuna WanaMsumbujini wengi wanaoishi na waliozaliwa ambao wanaishi na Wazanzibari kama ndugu.

Kutokana na juhudi na hatua hizo, Dk. Shein alisema kuwa mashirikiano katika sekta kadhaa za maendeleo ni muhimu na ya msingi kwani yanaweza kuleta tija na mafanikio zaidi kwa pande zote.

Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa mafanikio makubwa iliyoyapata Msumbiji katika kuimarisha uchumi wake sambamba na mafanikio katika sekta nyengine za maendeleo.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana uhusiano na ushirikiano huo uliopo kati ya Msumbiji na Zanzibar na kueleza kuwa mashirikiano yanayoendelezwa yatasaidia katika  


uimarishwaji wa sekta za maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, gesi na mafuta, biashara, utalii na nyenginezo.

Akizungumzia kwa upande wa sekta ya elimu, Dk. Shen alisema kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwa na Vyuo Vikuu Vitatu hivi sasa na kusisitiza haja kwa Msumbiji kuleta wanafunzi wake ili kuja kusoma Zanzibar ikiwa ni pamoja na kujifunza Lugha ya Kiswahili kupitia Chuo chake Kikuu cha Taifa cha SUZA.

 


Post a Comment

0 Comments