Business

header ads

URUSI KUPIGA MARUFUKU UTARATIBU WA BABY BOXES

 

Urusi inafikiria kupiga marufuku maeneo maalum yanayotumiwa na akina mama kuwaweka watoto wao wachanga wasiowataka maarufu kama Baby Boxes.
Uamuzi huo umependekezwa na Seneta Elena Mizulina na kuungwa mkono na serikali lakini umekosolewa vikali na baadhi ya watu kwa madai kwamba, marufuku hiyo itaamanisha vifo vya watoto wachanga watakaotupwa kwenye majalala na vichakani.

Urusi ina maeneo hayo takriban 20 ambapo mama mzazi aliyejifungua anaweza kumuacha mtoto wake akiwa salama.
Serikali ya Urusi inasema inapaswa kushughulikia sababu zinazopelekea kutelekezwa kwa watoto wachanga kama kutoa huduma za uzazi wa mpango, ushauri nasaha na huduma za kijamii kwa mimba zisizotarajiwa.

Post a Comment

0 Comments