Business

header ads

UELEWA WA WANANCHI KUHUSU UKIMWI WAFIKIA ASILIMIA 90


Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imeyataka mashirika, wadau na taasisi zilizo katika mapambano dhidi Ukimwi kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hizo  na kuepuka kujiingiza katika shughuli za uanaharakati ambazo ni kinyume cha sheria.

Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na wadau mbalimbali walio katika mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa baadhi ya wadau, mashirika na taasisi zimekuwa zikifanya shughuli nje ya malengo ya awali ya kuanzishwa hali inayosababisha mgongano katika jamii na kutaka taasisi hizo kuendelea kujikita na kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ,uhamasishaji wa wananchi kupima kwa hiari VVU kwa lengo la kujua hali zao  ili waweze kujikinga na maambukizi  mapya ya  ugonjwa huo.

Dkt.Maboko  amesema hali ya uelewa wa wananchi juu ugonjwa wa Ukimwi imefikia asilimia 90 kwa kuwa watanzania sasa wanauelewa kuhusu ugonjwa huo na hali zao kutokana na kuongezeka kwa kampeni za uhamasishaji na elimu ya kujikinga na maambukizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Lulu Ng’wanakilala amesema Taasisi zinazosajiliwa kutoa huduma za kuzuia na kupunguza maambukizi dhidi ya Ukimwi kujiingiza kwenye shughuli za uanaharakati zinakwamisha na kupunguza juhudi za Serikali na wadau wengine  walio kwenye mapambano dhidi ya Ukimwi.

Post a Comment

0 Comments