Business

header ads

SULTANI KIPINGO: MAANA HALISI YA SALUTI YA MAJI (WATER SALUTE)

 
Na Sultani Kipingo
Utamaduni huu umekuwepo kwa siku nyingi, hata hapa Tanzania, lakini ujio wa moja ya ndege mbili aina ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kutoka Canada ndio kumezua maswali mengi kiasi hata ikabidi tufanye utafiti na kuja na majibu haya, maana upotoshaji na porojo vilitamalaki.


Kwa kawaida saluti ya maji (Water Canon Salutation) iliyofanyiwa ndege hiyo Jumanne Septemba 20, 2016 katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, hutolewa wakati wa sherehe za chombo cha usafiri kinapoanza kazi kwa mara ya kwanza ama kinapomaliza kwa mara ya mwisho.
Kwenye viwanja vya ndege magari ya Zimamoto husimama kila upande wa njia ya kupitia ndege na kuinyunyizia itapopita chini yake, huku maji yakiwa katika umbo la upanga wa sherehe kama ambavyo wanajeshi hufanya wakati za harusi ya ofisa mwenzao.
Kwa mujibu wa utafiti wetu, saluti ya maji hutumika kumuaga rubani mwandamizi aliyestaafu, mungoza ndege ama safari ya kwanza ama ya mwisho ya ndege kwenye uwanja fulani ama ndege.
Saluti za maji hutumika pia hata kwa meli na vyombo vingine vya majini vinapoanza ama vinapomaliza kazi ama wakati wa kustaafu kwa nahodha mwandamizi.
 Katika utafiiti wetu tumegundua kwamba hii ni utamaduni wa kawaida kwenye bandari ama viwanja vya ndege ila sio sheria ama lazima. Inasemekana ilianzishwa miaka ya nyuma katika bandari ya New York nchini Marekani wakati wa kukaribisha meli.
Mfano mwaka 1962 melivita ya SS France (baadaye ikaitwa Norway) ilipewa ukaribisho wa saluti ya maji, kitendo ambacho kwa kuwa kilikuwa cha kuvutia kiliendelea kila mara meli ngeni ama mgeni mkubwa akifika bandarini hapo.
Mwaka 1936 meli ya Unigereza RMS Queen Mary ilipata mapokezi hayo.
Na mbali ya kuwa saluti ya maji kuwa ya kusherehekea mwanzo ama mwishop wa chombo ama nahodha, zoezi hilo pia hutumika kufanyia majaribio vifaa hivyo vya kuzimia moto.

Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments