Business

header ads

SIKU 14 ZA KUHAKIKI WATUMISHI WAUMMA KUANZA OKTOBA 3Serikali inatarajia kuendesha zoezi la uhakiki wa Watumishi wa umma kote nchini kwa siku 14 kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuondoa watumishi hewa na wenye utambulisho danganyifu.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejmenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Angellah Kairuki amesema zoezi hilo litahusisha uchukuwaji wa alama za vidole, vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa na hati ya malipo ya mshahara, Hati ya kusafiria, kadi ya mpiga kura na Kitambulisho cha Kazi.

Mhe. Kairuki amesema lengo nikuuimarisha mifumo ya usimamizi wa raslimaliwatu na mishahara kwakutumia kanzi data ya utambulisho wa Taifa ambapombo zoezi hilo litaendeshwa na mamlatka ya vimbulishi vya taifa na kwamba zoezi hilo litaanza Octoba 3.2016.

Aidha Mhe Kairuki amewataka Watumishi kote nchini katika Wizara mbalimbali, Idara za serikali zinazojitegemea, Tawala za Mikoa na mamlaka za serikali za mitaa, Wakala za Serikali, Taasisi na mashirika ya Umma ambapo zoezi zitahusisha na watrumishi wa serikali kwa upende wa Zanzibar


Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments