Business

header ads

SHILINGI BILIONI 170 KUTATUA KERO YA MAJI TANDAHIMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kitema I wilayani Tandahimba  waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili kwenye wilaya hiyo ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi na Mdhibiti wa ubora wa bidhaa Bw. Karim Hassan (kushoto) ya hatua mbali mbali ambazo korosho hupitia wakati wa kubanguliwa kwenye kiwanda cha AMAMA kilichopo Tandahimba mkoani Mtwara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imetenga zaidi ya bilioni 170 kwa ajili ya utekeleza wa mradi mkubwa wa maji kwa  wakazi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara hiyo ili kuondoa tatizo la uhaba wa maji uliodumu kwa kipindi kirefu.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tandahimba na wakati akihitimisha ziara yake ya siku NNE mkoani Mtwara ambapo amesema mkakati utaondoa usumbufu wa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Kuhusu usafirishaji wa korosho kwa njia ya magendo, Makamu wa amesema kuwa biashara ya magendo ya korosho inainyima serikali mapato mengi ambayo yangesaidia shughuli za maendeleo za wananchi hivyo mbapo ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mtwara uchukue hatua za kukomesha biashara hiyo haramu.

Akiwa mjini Tandahimba, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi la utoaji wa zawadi mbalimbali kwa uongozi wa shule ya sekondari ya Tandahimba kwa kuingia katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita ambapo Kampuni ya Startimes imetoa hundi ya shilingi milioni Mbili kwajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments