Business

header ads

SERIKALI KUTOA ELIMU KWA WOTE KUONDOA TABAKA LA WASIOJUA KUSOMASerikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejizatiti kuondoa tabaka la wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na watu wazima kwa kujenga uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa watu wote.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Duniani, yaliyofanyika leo, katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

“Wizara imejipanga vizuri, na lengo kubwa la wizara ni kuhakikisha tunakuwa na mtanzania aliye elimika na aliye na stadi, maarifa na uwezo wa kutumia elimu aliyoipata,” alifafanua Bureta.

Vile vile Bw. Bureta amesema kwa sasa wizara ipo kwenye mpango wa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ambao unaanzia chini kwa wanafunzi wa awali mpaka shule za msingi.

Katika mpango huo walimu wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya namna ya kumuwezesha mwanafunzi kujua Kusoma Kuandika na Kuhesabu katika ngazi ya elimu ya awali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina Levira amesema kwamba kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, asilimia 78 ya vijana na watu wazima ndio waliokuwa wakijua kusoma na kuandika.

Akaongeza kuwa mwaka 2015 idadi hiyo ya wanaojua kusoma na kuandika ilishuka na kufikia asilimia 77 ambapo ilipelekea wizara hiyo kutoka na mikakati inayokusudia kuondoa kabisa tabaka la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini.

Aidha, Basilina amesema kuwa Serikali ilipitisha sheria ya vyumba vya madarasa ya shule zote nchini kutumika kufundishia vijana na watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika muda wa jioni baada ya wanafunzi wa kawaida wanapomaliza masomo yao.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishugulisha na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Zulmira Rodrigers amesema kuwekeza kwa vijana waleo na watu wazima itaisaidia Tanzania kuondokana na theluthi moja ya watu wake wasiojua kusoma huku akitaka kuwekwa kwa utaratibu maalumu utakao wawezesha watoto milioni 3.5 ambao wako nje ya mfumo wa elimu kurudishwa shuleni

Kwa upande wake Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema wakati umefika kwa Tanzania kuhakikisha inatoa elimu bora na kutatua chanagamoto za upatikanaji wa elimu kwa watoto wakike ambao ndio waathirika wakubwa kwa kukosa elimu jambo ambalo litachochea lengo namba nne la maendeleo endelevu.

Post a Comment

0 Comments