Business

header ads

RAIS DKT.MAGUFULI ATOA MIEZI MIWILI KUANZA KWA UJENZI WA NYUMBA KWA WAKAZI WA MAGOMENI KOTA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waojenga mabweni hayo kutoka TBA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiangalia kwa furaha maendeleo ya ujenzi wa mabweni hayo unavyoendelea kwa kasi katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Mabweni hayo.

HABARI KAMILI

Rais wa Jamhuri ya muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehidi kumalizia kiasi cha bilioni tano alichoahidi katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuahiadi ajira kwa watendaji wa ujenzi huo.


Rais Magufuli ameyasema hay oleo wakati wa ziara yake katika eneo la Mlimani City ambapo kunafanyika ujenzi wa mabweni hayo ambapo amesema amefurahi kuona kuwa wakandarasi wa ndani wakijenga kwa gharama nafuu na kuwa Tanzania kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuhifadhi wanafunzi zaidi ya 4000.

Kwa upande mwingine Dkt. Magufulli ameipongeza TBA ambao ni wakandarasi wa ujenzi huo kwa kukubali kujenga mabweni hayo kwa gharama ya Bilioni kumi ujenzi unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka na kuwataka kuwatumia vijana wanaotekeleza mradi huo katika miradi mingine.
 

 KATIKA ZIARA YA PILI YA RAIS MAGUFULI MAPEMA LEO
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea taarifa ya wakazi wa magomeni kota iliyosomwa kwake na mchungaji John Raymond wakati Rais alipotembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam  Septemba 6, 2016. PICHA NA IKULU


HABARI KAMILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota kukaa kwenye nyumba za Serikali miaka mitano bure na baadaye kuzinunua kwa bei nafuu.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wakazi wa Magomeni ambapo amewataka wakandarasi katika kipindi cha miezi miwili waanze kujenga nyumba 644 kwa ajili ya wazee ambao wameteseka  baada ya nyumba zao kuvunjwa.

Ameongeza kusema kuwa ujenzi huu anataka ukamilike ndani ya mwaka mmoja au miezi sita kama ulivyokuwa kwa hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kueleza kuwa  atafurahi kukabidhi hati kwa wakazi wa Magomeni Kota pindi nyumba hizo zitakapokuwa zimekamilika.

“Namuomba Mwenyezi Mungu anipe uzima ili nyumba hizo zikiwa tayari hati nizikabidhi mwenyewe,”alisema Magufuli.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi, Mhe. William Lukuvi amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali wanyonge hasa kwa kutatua mgogoro wa makazi kwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Mheshimiwa Rais ninakushukuru kwa kuwajali wazee hawa wa Magomeni, nami nilitekeleza maagizo yako na kufuatilia mgogoro huu hadi kupata ufumbuzi”, alisema Lukuvi.
Lukuvi amesema kuwa mgogoro wa Magomeni ulivyokuwa mkubwa ulistahili nguvu ya Mhe. Rais Magufuli, lakini kwa migogoro mingine ambayo ni midogo, hiyo ameishughulikia na ataendelea kuishughulikia ili kero za wananchi kuhusu ardhi ziishe kama alivyoagizwa na Rais.

Nyumba zilizokuwa Magomeni Kota zilivunjwa mwaka 2009 na wananchi wakaahidiwa kujengewa nyumba ambazo wangeuziwa kwa bei nafuu. Lakini kwa takribani miaka mitano nyumba hizo hazikujengwa hali ambayo iliwafanya wakazi hao waishi maisha ya kuangaika.


Post a Comment

0 Comments