Business

header ads

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MBILI MPYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada  kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  wakitoka kwenye  ndege mojawapo na kuelekea ingine baada  kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam  Septemba 28, 2016

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amezindua rasmi ndege mbili mpya za ATCL aina ya Bombardier Q400 na kusema kuwa serikali bado inampango wa kununua ndege nyingine kubwa mbili mpya na fedha ya kununua ipo.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo leo Jijini Dar es Salaam, Rais Dk. Magufuli ameonyesha kusikitishwa na watu waliokuwa wakizibeza ununuzi wa ndege hizo, wakisema zinamwendo wa Bajaji, na kuhoji iwapo hivyo ni kweli ziliwezaje kutoka Canada hadi kuja Tanzania.

Kuhusu ununuzi wa ndege mbili kubwa mpya Dk. Magufuli amesema serikali itanunua ndege moja yenye uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine abiria 240 zenye uwezo wa kutoka Marekani, China na Uingereza moja kwa moja hadi Tanzania ili kuleta watalii.

Aidha, Dk. Magufuli alibainisha madhambi ya lililokuwa Shirika la ATC, ikiwemo ya kujiendesha kwa kuitegenea serikali, kutojiendesha kibiashara, shirika halizingatii uweledi, wafanyakazi wanafanya kazi kimazoea pamoja na ubadhirifu wa aina mbalimbali, na kuonya kuwa mwendo wa mchezo sasa umekwisha.

Post a Comment

0 Comments