Business

header ads

RAIS DKT. MAGUFULI AAGIZA KULIPWA KWA SHILINGI MILIONI 609 ZINAZODAIWA NA WAFANYAKAZI WA UHURU


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Magazeti hayo zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kushoto pamoja na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka mara baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakielekea kwenye Ofisi za Magazeti ya Uhuru na Mzalendo zilizopo katika mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru na kuagiza kulipwa kwa mishahara ya shilingi milioni 609 inayodaiwa na wafanyakazi wake.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana kuhakikisha mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia Shilingi Milioni 609 inalipwa ndani ya Mwezi huu wa Tisa, ameagiza kupatiwa orodha ya taasisi za Serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia ameagiza deni linalodaiwa na NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi lilipwe.

Rais Dkt. Magufuli ameahidi kufanyia kazi malalamiko dhidi ya Bodi na Menejimenti ya Kampuni hiyo, ajira za wafanyakazi, mafao kwa wastaafu, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti na mazingira magumu ya kazi Dkt. Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi.

Awali wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam wamelalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutotolewa kwa michango ya wafanyakazi kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za Serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.

Aidha, Dkt. Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa na amewakikishia kuwa anatambua umuhimu wao na kwamba atahakikishia anaboresha hali ya chombo hicho muhimu.


Wakati huo huo, Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.


Bonyeza HAPA kudownload application ya Elikunda, Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments