Business

header ads

MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkaoni Arusha imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini.

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo an Wakili wa Serekali Lilian Mmasi ni kosa la kutuhumiwa kujifanya Afisa Mtumishi wa Upelelezi wa (TISS) na kosa la pili ikiwa kughushi moja ya nyaraka za serekali (kitambulisho).

Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka yote, na ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwamkuga alipotoa masharti ya dhamana na mtuhumiwa kufanikiwa kuyatimiza.

Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeairishwa na Hakimu Mkazi Mwamkunga hadi itapotajwa tena Oktoba 5 ambapo uchunguzi unatarajiwa kuwa utakuwa umekamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.Mara baada ya kupata dhamana mahakamani hapo wakili wa mtuhumiwa Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi ukikamilika kesi itaanza kusikilizwa mapema na haki kutendeka ,huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.

“kwakweli kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru jeshi la polisi kwa kunishikilia na kukaa na mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana

Alisema kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuwa  wakitumia mali za umoja huo kujinufaisha wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.

Bonyeza HAPA kudownload application ya ELIKUNDA Ungana nami Elikunda Materu, kupata habari mbalimbali kutoka pande zote za dunia kupitia simu yako ya kiganjani.

Post a Comment

0 Comments