Business

header ads

HUDUMA YA UMEME VIJIJINI YAPANDA TOKA 2% HADI 41%

Idadi ya wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanaopata huduma ya umeme imeongezeka kutoka 2% mwaka 2007 hadi 41% mwaka 2016, ambapo kitaifa watu wanaopata huduma hiyo wameongezeka kutoka 10% 2007 hadi 58% .

Takwimu hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, (REA), Mhandisi Gissima Nyamohanga, ambaye amesema takwimu zinaonesha kati ya vijiji zaidi ya elfu 12 nchi nzima, vijiji 7,873 ndio havina huduma ya umeme.

Amefafanua kwamba, REA imeanza utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu wa kusambaza umeme vijijini unaotekelezwa kwa miaka mitano na kwamba hadi kufikia mwaka 2021 vijiji vyote nchini vitakuwa vimepatiwa nishati ya umeme.

Post a Comment

0 Comments