Business

header ads

GAVANA WA TANZANIA AKANUSHA KUWEPO KWA MDORORO WA UCHUMI


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu, amekanusha kuwepo kwa mdororo wa uchumi nchini, na kusema kuwa uchumi wa nchi unaendelea kukuwa kama ilivyotarajiwa.

Prof. Ndulu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia hali ya uchumi nchini, ambapo amesema uagizaji wa malighafi za viwandani nao umeongezeka kwa asilimia 19.4.

Akizungumzia kuhusu mzunguko wa fedha nchini, Prof. Ndulu amesema fedha zimehama kutoka katika mikono haramu kwenda kwenye matumizi halali na sahihi kwa umma.

Profesa Ndulu pia amesema Serikali haina mpango wa kuchapicha noti mpya kwa sababu uchumi wa nchi ni imara na hakuna sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments