Business

header ads

DKT.DAU AAPISHWA KUWA BALOZI WA TANZANIA MALAWIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo amemuapisha Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia. 

Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF). 

 Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Post a Comment

0 Comments