Business

header ads

BAGENI AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFAMahakama ya Rufaa imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, OC–CID, Christopher Bageni, baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

Wakati Bageni akihukumiwa kunyongwa, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar es Salaam RCO, Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wa polisi ambao ni Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa huru baada ya mahakama kuwaona hawana hatia.
Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwauwa kwa makusudi wafanayabiashara wa madini Sabinus Chigumbi, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu aliyekuwa dereva teksi wa Manzese.
Mauaji hayo yalifanyika Januari 14 mwaka 2006 katika msitu wa Pande wilaya ya Kinondoni baada ya wafanyabiashara hao kukamatwa eneo la Sinza walipokuja kwa shuguli za kibiashara.

Post a Comment

0 Comments