Business

header ads

Ali Bongo ASEMA YUKO TAYARI KUTII UAMUZI WA MAHAKAMA


Rais wa Gabon, Ali Bongo, amesema yuko tayari kutii uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba iwapo mahakama hiyo itaamuru kura za uchaguzi mkuu uliofanyika wiki mbili zilizopita zihesabiwe upya.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuna kasoro nyingi kwenye matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa, ambayo yalimpa Rais Bongo ushindi mwembamba.
Katika mahojiano na kituo cha redio cha Ufaransa, Rais Bongo amesema sheria za nchi yake haziruhusu kura zihesabiwe upya lakini akasema, atakubali iwapo mahakama itaamua hilo lifanyike.
Mahakama ya kikatiba inatarajiwa kukutana Alhamisi kupitia kesi ya kupinga matoke ya uchaguzi huo ambayo iliwasilishwa na mgombea wa upinzani, Jean Ping.

Post a Comment

0 Comments