Business

header ads

WAZIRI WA ELIMU, PROF. JOYCE NDALICHAKO AITAKA VETA KUPITIA UPYA MITAALAmwalimu wa Ufundi Ricky akionyesha baadhi ya mashine zinazotumika kufundishia wanafuinzi wanaojiunga na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kIPAWA

Picha ya pamoja kayi ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof  Joyce Ndalichako akiwa na watendaji wa Chuo cha VETA Kipawa pamoja na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof  Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya mikakati ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda ambapo chuo cha VETA Kipawa inajikita zaidi kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya viwanda

mmoja wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mlimani waliokwenda chuoni hapo kupata mafunzo kwa vitendo juu ya masuala ya TEHAMA


Habari/Picha Beatrice Lyimo-MAELEZO

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka Menejimenti ya Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia upya mitaala na vifaa vilivyopo katika vyuo vyote nchini ili kuweza kukidhi mahitaji ya kisasa.

Waziri Ndalichako aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kutembelea Chuo cha mafunzo na ufundi stadi kituo cha VETA kilichopo Kipawa ili kujionea maendeleo ya chuo hicho na mafunzo yanayotolewa.

Alisema katika ziara zake katika vyuo mbalimbali vya VETA nchini amebaini baadhi ya vifaa mbalimbali ikiwemo kuna baadhi ya mashine kuwa hazitumiki kulingana na mahitaji ya chuo.

“Nawataka Menejimenti katika vyuo vyote vya VETA nchini kupitia mitaala na vifaa vilivyopo ikiwemo mashine katika kila chuo ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo ili vyuo hivyo vilingane katika ubora wa mafunzo yanayotolewa kila mkoa”alisema Prof. Ndalichako.

Akifafanua zaidi Prof. Ndalichako alisema adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vijana wanaajiriwa na kujiajiri ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo na kutekeleza hitaji la Serikali ya Awamu ya Tano katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Geoffrey Sabuni alisema  VETA Kipawa ni chuo kinachoangaliwa kwa umakini zaidi kwani kinatoa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa ujumla kwa fani zinazolenga kuhudumia viwanda kwa hali ya juu.

Alisema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na  changamoto mbalimbali ikiwemo suala la utoro kwa wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo kwani baadhi yao huwa hawarudi na kupelekea wanafunzi wao kukosa vyeti vinavyoonyesha utaalamu walionao.

Post a Comment

0 Comments