Business

header ads

WATANGAZAJI MISRI WASIMAMISHWA KAZI KWA UNENETelevisheni ya Taifa ya Misri imewasimamisha kazi watangazaji wake wa kike wanane na kuwaamuru kupunguza unene hali iliyozua malalamiko kutoka kwa makundi yanayotetea haki za wanawake nchini humo.

Umoja wa Radio na Televisheni wa Misri, umewapa muda wa mwezi mmoja watangazaji hao kupunguza unene kabla ya kuruhusiwa tema kutangaza kwenye runinga.
Kwa mujibu wa tovuti ya Al – Yawm al – Sabi, Mkurugenzi wa umoja huo ni mwanamke, Bi. Safaa Hegazy, ambaye binafsi alikuwa mtangazaji wa runinga amewashangaza wengi kwa uamuzi aliochukua.

Mmoja wa watangazaji waliokumbwa na mkasa huo Bi. Khadija Khattab, amewataka watu kuangalia vipindi vyake vya hivi karibuni na waamue kama kweli ni mnene kiasi hicho na kustahili adhabu aliyopewa.

Post a Comment

0 Comments